Header Ads

ad

Breaking News

Kocha wa Azam FC aomba kibarua Malawi

Caps: Kocha John Stewart Hall (kulia), akiwa na Mwenyekiti wa Azam FC, Mohamed Saidi, wakati wa kuingia naye mkataba wa kuifundisha timu hiyo.

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Hall Stewart ameamua kuitosa timu hiyo na kuomba kazi kuifundisha timu ya taifa ya Malawi 'The Frames'.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), ilieleza kwamba Stewart ni miongoni mwa makocha walioomba nafasi ya kuinoa timu hiyo.

Ofisa Habari wa Azam, Jaffar Idd, amesema uongozi wa timu hiyo umempa baraka zote kocha huyo katika mpango wake huo.

"Ni kweli kocha wetu (Stewart) ni mmoja wa makocha duniani walioomba nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya Malawi, hilo ni jambo zuri kwani tuna amini ana uwezo wa juu wa kufundisha.

Amesema Stewart, ana elimu ya kutosha ya kufundisha timu yoyote kwani ni Mkufunzi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Amesema endapo akifanikiwa kuchaguliwa kufundisha timu hiyo, watakaa naye chini kuzungumza upya.

Kocha huyo alijiunga na Azam FC, tangu msimu uliopita baada ya kuiwezesha Zanzibar Heroes kuonesha kiwango kizuri katika michuano ya Kombe la Chalenji, ambapo Taifa Stars ilitwaa ubingwa huo.

No comments