Header Ads

ad

Breaking News

Stars kuagwa Alhamisi


TIMU ya taifa 'Taifa Stars, inatarajia kuagwa kesho kwa ajili ya safari yao ya kwenda mjini Marrakech, Morocco kukamilisha mchezo wa mwisho wa Kundi D wa kuwania kufuzu Mataifa ya Afrika, mwakani (CAN 2012).

Fainali hizo zitafanyika katika nchi za Guinea ya Ikweta na Gabon, ambapo kundi hilo linaongozwa na Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati zikiwiana kwa pointi nane zikifuatiwa na Taifa Stars na Algeria zenye pointi tano kila moja.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema timu hiyo itaagwa saa 4 asubuhi kambini kwao jijini Dar es Salaam.

Amesema mechi hiyo itapigwa Jumapili na kwamba tayari wachezaji watano wanaocheza nje ya nchi, wamearipoti kambini.

Amewataja wachezaji hao ni Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya, Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden).

Ameongeza kuwa, wachezaji wanaocheza Vietnam, Abdi Kassim na Dan Mrwanda, wanatarajia kuwasili nchini kesho mchana majira ya saa nane.

No comments