Header Ads

ad

Breaking News

BFT, Kenya kuwapambanisha vijana wa kiume, wa kike


SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), likishirikiana na Shirikisho la Ngumi la Kenya, wanatarajia kuendesha mashindano ya kusaka vipaji vya vijana vya ngumi hizo Desema 14 hadi 20, mwaka huu nchini.

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga amesema mashindano hayo yatashirikisha vijana wa kiume na wa kike kwa lengo la kutafuta timu ya taifa ya vijana, ambayo itaiwakilisha nchi katika michuano mbalimbali.

 Mashaga amesema kwa sasa wapo katika mchakato wa kuangalia sehemu ya kufanyia mashindano hayo, ambayo itakuwa kati ya Arusha au Dar es Salaam.

Amesema kwa sasa wamejipanga kwenda kulingana na Baraza jipya la Michezo la Taifa (BMT), katika kuhakikisha michezo yote inakuwa na kuleta mafanikio kwenye mchezo husika.

No comments