Header Ads

ad

Breaking News

Waziri mgeni rasmi maonesho ya ubunifu kesho

                                                              Waziri Sophia Simba

WAZIRI wa Maendeleo, Jinsia na Watoto, Sophia Simba kesho atazindua maonesho ya ubunifu wa mavazi ya TWINDWE yatakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Maonesho hayo yaliyoandaliwa na mbunifu wa mavazi, Mustapha Hasanali kwa kushirikiana na wajasiriamali mbalimbali yatafanyika sambamba na Semina ya ubunifu na ujasiriamali.

Meneja wa Mradi wa TWENDE, Gloria Mongela, amesema maonesho hayo yatawakunatisha wabunifu wa mavazi na wajasiriamali kutoka mikoa sita ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema mikoa itakayotoa wabunifu na wajasiriamali ni Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro, Tabora, Iringa na wengine wanatoka Zanzibar.

Maonesho hayo yatafanyika kwa siku tatu, ambapo wabunifu na wajasiriamali 70 watahudhuria maonesho hayo.

No comments