Fainali ya Airtel Rising kuanza kuchezwa Jumamosi
Ofisa habari wa Kampuni ya Simu za mkononi Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), Boniface Wambura (TFF), Iddi Mshangama (TFF).
TIMU za soka za vijana wenye umri chini ya miaka 17 za mikoa ya Mwanza na Morogoro, zinatarajia kufungua pazia la fainali za michuano ya Airtel Rising Stars, itakayoanza Jumamosi Jijini Dar es Salaam.
Fainali hizo zitahusisha timu za mikoa minne ambayo ni Iringa, Morogoro, Dar es Salaam na Mwanza na zitamalizika Septemba 24 mwaka huu.
Ofisa Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Iddi Mshangama amesema kila siku utachezwa mchezo mmoja siku.
Amesema Iringa itacheza na wenyeji Dar es Salaam Jumapili katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Amesema mechi nyingine itakayopigwa Septemba 23, mwaka huu Mwanza watamenyana na Iringa ambapo mechi ya mwisho itachezwa Kati ya Morogoro na Dar es Salaam na kisha mshindi kutangazwa.
Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando amesema wachezaji sita watakaofanya vizuri watachaguliwa kuungana na wenzao sita kutoka kila nchi ya Afrika inayoendesha mashindano hayo katika kliniki itakayofanyika Oktoba 27 hadi Novemba 23 Dar es Salaam.
Mbanndo alisema wakufunzi kutoka katika klabu ya soka ya Manchester United ya Uingereza watakua nchini kuendesha kliniki hiyo ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa kituo cha kuendeshea kliniki hiyo.
Amesema timu zitakazoshiriki fainali hizo zitaanza kurejea Jijini Dar es Salaa kuanzia ijumaa ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa mshindi wa kwanza mpaka wa tatu.

No comments