Taifa Queens yaibamiza Afrika Kusini, ikishinda kesho kurejea na medali
TIMU ya taifa ya netiboli 'Taifa Queens', imeendelea kujisafishia njia ya kutwaa medali katika michuano ya Mataifa ya Afrika 'All Africa Games', baada ya jana kuifunga Afrika Kusini mabao 32-29.
Taifa Queens imeshuka dimbani jana, katika viwanja vya Zimpete ikiwa na kumbukumbu mbaya ya baada ya kuzi kufungwa na Uganda mabao 52-41.
Akizungumza kwa simu kutoka Maputo, Msumbiji Mkuu wa Msafara wa timu za Tanzania Henry Lihaya, amesema Taifa Queens ndiyo timu pekee inayoonesha matumaini ya kutwaa medali katika michuano hiyo.
Amesema baada ya ushindi huo, timu hiyo itamaliza kazi leo kwa kumenyana na Botswana katika mchezo wa mwisho ambao wanatakiwa kushinda kupata medali.
Katika mashindano hayo yanayochezwa kwa mtindo wa ligi, mshindi wa kwanza atanyakua medali ya dhahabu, wapili shaba na wa tatu fedha.
Taifa Queens tayari imecheza mechi saba ikiwa na pointi kumi ikiwa imeshinda mechi tano na kufungwa mbili.
No comments