Header Ads

ad

Breaking News

Waandishi 40 kupigwa msasa Sept. 25

 Meneja Uhusiano na Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu udhamini wa Vodacom wa sh. milioni saba kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA, kwa ajili ya semina kwa wanachama wake, pembeni yake ni Katibu Mkuu wa TASWA Amiri Mhando. 

WAANDISHI 40 wa habari za michezo nchini, wanatarajia kushiriki mafunzo ya awali ya siku mbili yaliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Tanzania (TASWA) Oktoba Mosi na 2, mwaka huu mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando, leo amesema mafunzo hayo ambayo awali yalipangwa kufanyika Septemba 24 na 25, mwaka huu yatahusisha waandishi kutoka mikoa mitatu ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani.

Amesema waandishi 25, watauwakilisha mkoa wa Dar es Salaam, ambapo Mkoa wa Morogoro utawakilishwa na waandishi 10 na wengine watano watatoka Pwani.

Mhando amesema michezo itakayopewa kipaumbele katika mafunzo hayo ya awali ni kikapu, wavu, na riadha na pia kwa sasa wapo katika harakati kuangalia uwezekano wa mchezo wa ngumi kushirikishwa.

Amesema wakufunzi watakaongoza mafunzo hayo ni sita (hawakutajwa), ambapo baadhi yao ni wahariri waandamizi wa michezo, wakufunzi katika vyuo mbalimbali vya uandishi, pamoja na wanasheria wa masuala ya habari.

Katibu huyo amesema mafunzo hayo yatafuatiwa na mengine, yatakayofanyika Novemba mwaka huu kwa waandishi wa mikoa ya Manyara, Tanga na Kilimanjaro ambapo wahariri wa vyombo vya habari nao watashiriki mafunzo Desemba mwaka huu.

No comments