Header Ads

ad

Breaking News

Simba, POlisi Dodoma zaingiza 16, 839,000/-

Msemaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),  Boneface Wambura, amesema mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Polisi Dodoma iliyochezwa juzi Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam imeingiza sh. 16,839,000.

Msemaji huyo wa TFF amesema watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo walikuwa 2,257, ambapo kiingilio kilikuwa sh, 7,000 kwa mzunguko na sh. 20,000 kwa viti maalumu (VIP) na waliokata tiketi za sh. 20,000 walikuwa 80.

Amesema baada ya kuondoa gharama za mchezo na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo ni sh. 2,568,661.02 kila timu ilipata sh. 3,546,671.90 na mgawo mwingine ulikwenda kwa uwanja sh. 1,162,893.

Wambura amesema TFF ilichukua sh. 1,162,893, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 581,446, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 465,157 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 116,289.39.

No comments