Header Ads

ad

Breaking News

Rage, Sendeu kikaangoni Sept.24

 Mwenekiti Simba, Ismail Aden Rage          Msemaji Yanga, Louis Sendeu

KAMATI ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepanga kukutana Septemba 24, mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mashauri matatu dhidi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage na Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu.

Viongozi hao watafikishwa mbele ya kamati hiyo, kutokana na kuyumbisha mchezo wa Ngao ya Jamii kwa nyakati tofauti, kitendo ambacho kinadaiwa kiliathiri uingiaji wa watu katika mchezo huo kutokana na kauli walizotoa.

Rage alidai kuna kiongozi TFF, anakwamisha mchezaji wao Gervais Kago, asisajiliwe kwa wakati na Sendeu yeye ana mashtaka mawili la kuyumbisha mchezo pamoja na kumtolea lugha, inayoonekana kumsababishia matatizo mwamuzi Alex Mahagi, katika maisha ya kila siku.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo na Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura amesema awali kamati hiyo chini ya Mwenyekiti, Alfred Tibaigana ilikuwa ikutane Agosti 29, mwaka huu kusikiliza malalamiko ya TFF dhidi ya viongozi hao, lakini kikao kiliahirishwa kutokana na Kamati kutotimiza akidi (column) kwa wajumbe wake.
 
Amesema shirikisho hilo, liliwasilisha shauri jipya dhidi ya Sendeu, kutokana na matamshi yake dhidi ya mwamuzi Mahagi aliyechezesha mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting iliyochezwa Septemba 10, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
 
Amesema Sendeu alimshutumu Mahagi kuwa alisababisha timu yake, ikose ushindi kwa kuwabeba wapinzani wao na anamfahamu Mahagi kuwa ni mwanachama wa Simba na kadi nyekundu aliyompa kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima haikuwa halali.

No comments