Tamasha la sanaa Bagamoyo kufungwa Jumamosi
Maonesho ya 30 ya Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni wa Mtanzania litafungwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangara, kesho kwenye viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA).
Mwenyekiti wa tamasha hilo, Bafadhil Bura, amesema kuwa, maonesho hayo yatafungwa jioni sambamba na kufanyika kwa mahafali ya wasanii wa mwaka wa tatu waliohitimu mafunzo chuoni hapo.
Amesema kutakuwa na maonesho mbalimbali ya ngoma za asili, sarakasi, maigizo na muziki zikiongozwa na wasanii wa Splended Theatre kutoka jijini Dar es Salaam.
Pia, wenyeji TASUBA na nguli wa reggae nchini, jhiko Manyika, atapanda jukwaani kuwaburudisha.
Bura amesema vikundi na wasanii mmoja mmoja, watapata utambulisho kama walishiriki
maonesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka.
Amesisitiza kuwa, wasanii wanatakiwa wafahamu kama tamasha la Sanaa Bagamoyo ni lao na wanapashwa kujiandaa ili maonesho yao yawe na mvuto.
No comments