TASWA kuzindua viwanja Kigamboni, yasaidiwa jezi
Mratibu na Afisa Habari wa hifadhi ya Dar es Salaam Zoo, Abdallah Bawazir (kulia), akimkabidhi jezi Mwenyekiti wa TASWA FC, Majuto Omary, kwa ajili ya mechi ya itakayochezwa Uwanja wa Dar es Salaam Zoo, kesho. Foto: TASWA FC
HIFADHI ya wanyama pori ya Dar es Salaam Zoo, leo itazindua viwanja vya michezo vilivyopo katika hifandhi hiyo ambapo imealika timu ya TASWA FC kucheza nayo mechi ya kirafiki. Leo wamekabidhiwa jezi na hifadhi hiyo.
Viwanja vitakavyozinduliwa katika hifadhi hiyo ya wanyama pori, iliyopo Kigamboni, nje kidogo ya Dar es Salaam ni vya soka, kriketi, mpira wa mikono na tenisi.
Mkurugenzi wa Dar es Salaa Zoo Abdallah Bawazir, amesema viwanja hivyo vitatumika katika michezo na mabonanza mbalimbali.
Amesema mbali na mechi hiyo, pia TASWA FC itapata nafasi ya kutembelea wanyama waliopo kwenye mbuga hiyo, ili kutoa elimu kwa Watanzania kupitia taaluma zao.
Mwenyekiti wa TASWA FC Majuto Omari, ameishukuru hifadhi hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwaalika katika kuzindua viwanja hivyo na kuwaomba pia kuendelea kutoa michango kwa timu hiyo, pamoja na ya netiboli ambayo inahitaji msaada huo ili ijiimarishe.

No comments