Mlawa awaita wasanii kumlaki Mama Samia
Na Omary Mngindo, Kiwangwa
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Aboubakary Mlawa, amewaita Wasanii kufika kwa wingi kumlaki Rais Dkt. Samia Suluhu.
Mlawa alitoa Rai hiyo katika Uzinduzi wa Kampeni ya Udiwani Kata ya Kiwangwa mbele ya Mgombea Ubunge, Ridhiwani Kikwete, kabla ya kumnadi Malota Kwaga.
Alitoa rai hiyo baada ya kushuhudia Wasanii kutoka vikundi mbalimbali walipotumbuiza kwenye uzinduzi huo, ambapo alielezea kufurahishwa kwake kwa kazi nzuri ya Wasanii hao.
Alisema kuwa kwa nafasi yao wasanii wanasaidia kukonga nyoyo za wananchi wanaofika kwenye sherehe mbalimbali, ambapo burudani zao zinawaondolea uchovu wanaohudhuria tukio
"Siku ambayo Mgombea wetu wa Urais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan atakapokuja Chalinze, itapendeza sana nikiwaona wasanii wakijitokeza kwa wingi wao," alisema Mlawa.
Malota KwagaAkizungumza na mwandishi wa habari hizo baada ya mkutano huo, Kwaga alisema kuwa ndani ya Kata hiyo kuna Wasanii wengi vijana na kwamba amekuwa nao karibuni katika kuendeleza vipaji hivyo.
"Vikundi vyangu vinaendelea na utoaji wa burudani katika shughuli mbalimbali ndani ya Kiwangwa na nje pale wanapohitajika, nawashukuru kwa kuendeleza burudani katani kwangu," alisema Kwaga.
No comments