Darasa la nne Innovate netiboli yashinda 2-1
Na Omary Mngindo, Kibwende
TIMU za Netiboli katika shule ya Awali na Msingi ya Innovate kati ya darasa la nne na la tatu zimechuana kwenye mchezo Maalumu uliochezwa shuleni hapo.
Katika mchezo huo ukiwa ni mwendelezo wa michezo shuleni hapo kila Ijumaa ya wiki, timu ya netiboli darasa la nne imeibuka na ushindi wa goli 2 - 1.
Kwenye mchezo huo uliochezeshwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Said Chande (Sir Side), magoli yote ya washindi yamefungwa na mchezaji Yassinta Evans huku bao pekee la Darasa la tatu likifungwa na Braitnes Yussuf.
Katika upande wa soka darasa la nne imeibuka na ushindi wa bao moja-0a, likiwekwa wavuni na Renatus Sumbi, akiunganisha mpira uliopigwa kutoka pembeni mwa uwanja.
Alisema kuwa, shule yao mbali ya taaluma pia imekuwa mstari wa mbele kuibua vipaji vya wanafunzi katika nyanja za michezo, sanaa na burudani na ushahidi huo unadhihirishwa na ushindi wanaopata katika shule mbalimbali
"Shule yetu imekuwa ikishiriki katika michezo mbalimbali katika shule tofauti, na tumekuwa tukifanya vizuri katika michezo hiyo, niwaombe wazazi waviendeleze vipaji hivyo," alisema Mwalimu Chande.
Chande alimalizia kwa kuwaomba wakazi wa Kibwende na Vitongoji vyake kuendelea kuiunga mkono shule hiyo chini ya Mkurugenzi wake, George Ndaki, ambaye ameamua kujenga shule hiyo akilenga kusaidia jamii ya wana Kibwende.
No comments