MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI MATOFALI 41,000 NA SARUJI TANI 102 KUCHOCHEA SHUGHULI ZA MAENDELEO DODOMA JIJI
Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde (wa nne kutoka kulia), akikabidhi mifuko tani 102 ya saruji kwa kata 41 za jimbo hilo leo Alhamisi Mei 22,2025
Ni kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi kwa kata zote 41
Jiji la Dodoma latenga bilioni 6 kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi
Vifaa kulenga kuboresha sekta ya afya na elimu
Rais Samia apongezwa kwa maendeleo makubwa Dodoma Jiji
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Kamati ya Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo na Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde leo Alhamisi Mei 22,2025 amekabidhi matofali 41,000 na saruji tani 102 kwa kata zote 41 za Dodoma Mjini kwa lengo la kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya Elimu na vituo vya Afya.
“Mfuko wa Jimbo hujielekeza katika miradi ya kipaumbele ya elimu, afya na uwezeshwaji wananchi kiuchumi.
Leo tunakabidhi matofali na saruji kwa kata zote 41 kwa lengo la kuunga mkono miradi inayoibuliwa na wananchi.
Kwa sasa Jiji la Dodoma limetenga shilingi bilioni 6 kuunga mkono miradi yote inayoibuliwa na wananchi ili kuchochea maendeleo zaidi ndani ya Dodoma Jiji.
"Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa sana ya kuiendeleza Dodoma hivyo ni wajibu kazi hii nzuri kuungwa mkono kwa wivu mkubwa,”alisema Mavunde.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma, Charles Mamba, wamepongeza hatua ya Mfuko wa Jimbo kujibu mahitaji ya jamii na hasa katika kuboresha sekta ya elimu na afya na hivyo kusaidia kusogeza maendeleo kwa wananchi kwa ukaribu zaidi.
Akitoa taarifa ya mfuko wa Jimbo, Mratibu wa Mfuko, Debora Muwinje amesema mfuko wa Jimbo la Dodoma Mjini unapokea kiasi cha shilingi milioni 93 kuchochea maendeleo, kiasi ambacho kimetumika na kugharamia mahitaji ya vifaa husika na kumpongeza Mbunge Mavunde kwa kuchangia mifuko ya saruji 1,000 ya ziada ili kuhakikisha eneo kubwa zaidi linaguswa.

Mbunge wa Dodoma Mjini Anthony Mavunde (katikati), akikabidhi moja ya matofali kati ya matofali 41,000 kwa kata 41 za jimbo hilo leo Alhamisi Mei 22,2025

No comments