MADINI YA ALMASI YENYE THAMANI YA TSH 1.7 BILIONI YAKAMATWA YAKITOROSHWA UWANJA WA NDEGE MWANZA
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa jijini Mwanza Mei 23,2025




Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MADINI ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari ljumaa usiku,Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda, vyombo vya usalama, uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya.
Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu zitakapokamilika.
Katika tukio hilo, almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67), yaligunduliwa yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.
No comments