Chalinze yatenga bilioni 2 kukopesha vikundi
Na Omary Mngindo, Chalinze
HALMASHAURI ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani imetenga kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kukopesha vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Hassani Mwinyikondo, akisema kwamba kikundi cha Mtetezi wa Mama baada ya Baraza la Madiwani kutenga kiasi hicho kupitia mapato yake ya ndani.
"Hapa halmashauri yenu tumetenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuwakopesha, mnachukua ile hela kwa kwenda kuifanyia malengo yaliyokusudiwa, sasa mkiogopa mnamuangusha Mheshimiwa Rais," amesema Mwinyikondo.
Aliongeza kuwa "Hamuwezi kuwa Mtetezi wa Mama wakati huna hela, wakati Mheshimiwa Rais Samia ana pesa ya kutosha, mpaka sasa halmashauri ya Chalinze tuna zaidi ya ahilingi bilioni mbili," alisema Mwenyekiti huyo.
Kwa upande Diwani wa Kata ya Bwilingu Nassa Karama amesema kuwa kikundi hicho kina malengo makubwa ya kimaendeleo, na kwamba anaimani nacho mpaka kufikia mwakani watakuwa wamefika mbali.
"Kwanza nikupongeze Mwenyekiti kwa maono yako ya mbali, lakini nami niseme kwamba sina maahaka na kikundi hiki kwani kimejipanga vilivyo, mpaka ifiapo mwakani Mbio za Mwenge wa Uhuru huenda zikatembelea moja ya miradi yake," amesema Karama.
Baada ya kauli ya Karama, Mwinyikondo amesema mwakani watakuwa wamechelewa badala yake watumie muda huu kuchangamkia fursa hiyo.
No comments