Mifugo yarudisha nyuma maendeleo ya Kijiji cha Kitonga
Na Omary Mngindo, Kitonga
WIMBI la Mifugo katika Kijiji cha Kitonga Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani, kimerudi nyuma kimaendeleo kufuatia wimbi la mifugo.
Kijiji hicho maarufu kwa kilimo cha mpunga wakulima waliowengi wamekimbia kuendeleza kilimo huku wakidaiwa kuelekea mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa wa Morogoro.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari kijijini hapo, wakazi Ally Yussuf, Abdallah Mpembenue na Fadhili Sato walisema kuwa kijiji kiazidi kudumaa kutokana na wimbi la mifugo.
"Kijiji chetu kilikuwa maarufu kwa kilimo cha mpunga, watu kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wa Kariakoo jijini Dar es Salaam walikuwa wanalima, kipindi hicho magari mawili yalikuwa yanapishana ili linalala lile linaondoka," alisema Yussufu.
Naye, Sato alisema kwamba Kijiji chao ni kwa ajili ya kilimo na si biashara, hivyo vijana wengi walikuwa wanajihusisha na kilimo lakini kutokana na wimbi hilo wengi wameacha kulima.
"Mifugo imekuwa kero kubwa, Mayumo (Mpembenue) amelima mpunga wake umekuwa mkubwa, pia amezungushia uzio lakini wameubunja ng'ombe wameingia wameula wote," alisema Sato.
Akizungumzia kero hiyo Mpembenue amwaomba viongozi ngazi ya Wilaya wafike kuwasikiliza kwani hali imekuwa mbaya, na kwamba amelima shamba kubwa lakini lote limeliwa na ng'ombe.
"Tumewaita Waandishi wa Habari mje mchukue kero yetu, Serikali inatuhimiza tulime wananchi tunalima lakini tunarudishwa nyuma na ng'ombe tunawaomba viongozi waje kutusaidia kuondokana na adha hii," alimalizia Mpembenue.
No comments