Mwandishi
Wetu
WEKUNDU wa
Msimbazi, Simba, jioni ya leo wameaga mashindano ya SportiPesa Super Cup kwa
matuta 5-4 dhidi ya Nakuru All Stars, mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam.
Simba ambao
ni mabingwa wa Kombe la FA, katika mchezo huo walitoshana nguvu na kutoka
suluhu dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya, hivyo inaungana na Singida United iliyokuwa
ya kwanza kutolewa ikafutiwa na Jang'ombe Boys iliyolazwa mabao 2-0 dhidi ya
vinara wa Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia.
Nakuru kwa
utemi wao huo, sasa itapepetana na wazee wao wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo
wa nusu fainali utaochezwa Alhamisi.
Penalti za
Simba zilifungwa na nahodha, Mwinyi Kazimoto, Besala Bukungu, Musa Hafidh na
Festo Munezero, wakati kipa Mghana Kipa, Daniel Agyei alikosa penalti yake
Nakuru wao
waliibuka na furaha kwa penalti zilizofungwa kiufundi na wachezaji wote watano
ambao ni Baraka Nturukundo, Amani Kyatta, Kangethe Maina, Ekuba Amakanji na
Kamau Ng'ang'a.
No comments:
Post a Comment