Header Ads

ad

Breaking News

Simba yapigwa kumbo michuano ya SportiPesa Cup








Mwandishi Wetu

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, jioni ya leo wameaga mashindano ya SportiPesa Super Cup kwa matuta 5-4 dhidi ya Nakuru All Stars, mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la FA, katika mchezo huo walitoshana nguvu na kutoka suluhu dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya, hivyo inaungana na Singida United iliyokuwa ya kwanza kutolewa ikafutiwa na Jang'ombe Boys iliyolazwa mabao 2-0 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia.

Nakuru kwa utemi wao huo, sasa itapepetana na wazee wao wa Kenya, Gor Mahia katika mchezo wa nusu fainali utaochezwa Alhamisi.

Penalti za Simba zilifungwa na nahodha, Mwinyi Kazimoto, Besala Bukungu, Musa Hafidh na Festo Munezero, wakati kipa Mghana Kipa, Daniel Agyei alikosa penalti yake

Nakuru wao waliibuka na furaha kwa penalti zilizofungwa kiufundi na wachezaji wote watano ambao ni Baraka Nturukundo, Amani Kyatta, Kangethe Maina, Ekuba Amakanji na Kamau Ng'ang'a.

No comments