Rwanda U20 yawasili kuikabili Ngorongoro Heroes
Ngorongoro Heroes |
TIMU ya taifa ya
Rwanda ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, imewasili jijini Dar es Salaam
jana, kwa ndege ya RwandAir kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya
Ngorongoro Heroes.
Rwanda yenye msafara
wa watu 27 wakiwemo wachezaji 20, itafikia hoteli ya Sapphire, ambapo mechi
hizo zitachezwa leo kwenye Uwanja wa Chamazi na Julai 16, mwaka huu Uwanja wa
Taifa.
Ngorongoro Heroes
tayari iko kambini chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Adolf
Rishard, kujiwinda kwa mechi hizo ambazo ni sehemu ya maandalizi ya kuivaa
Nigeria.
Mechi dhidi ya
Nigeria ambayo ni ya kwanza ya raundi ya pili kusaka tiketi ya kucheza fainali
za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Algeria itachezwa Julai 29 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments