Mwanza kucheza fainali Copa Coca Cola Jumapili
TIMU ya Mkoa wa Mwanza imekata tiketi ya kucheza fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 iyakayopigwa Jumapili, baada ya leo asubuhi kuilaza Temeke mabao 3-1, katika mchezo wa nusu fainali uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Hadi dakika 90
zinamalizika, timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Mwanza walipata bao
lao dakika ya tatu kupitia kwa Jamal Mtegeta, kabla ya Temeke kusawazisha kwa
penalti dakika ya 56, iliyowekwa wavuni na Baraka Ntalukundo.
Mabao mengine ya
Mwanza yaliyoipatia tiketi ya kucheza fainali kesho yalifunga dakika 30 za
nyongeza, kupitia kwa Mtegeta dakika ya 94, kabla ya Dickson Ambundo kukwamisha
la tatu dakika ya 108.
No comments