KIMANJARO PREMIUM LAGER YAKABIDHI SIMBA NA YANGA VIFAA VYA KOMBE LA KAGAME
Ikiwa ni sehemu ya
udhamini wake, Kilimanjaro Premium Lager imezikabidhi timu za Simba na Yanga
vifaa kwa ajili ya michuano ya Kombed la Kagame iliyopangwa kuanza wikendi hii
jijini Dar es salaam. Kaimu Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Oscar
Shelukindo alisema: “Bila shaka Simba na Yanga ni klabu kubwa zaidi nchini
Tanzania na zote kwa pamoja zimefika fainali za Kombe la Kagame mara 18, jambo
ambalo ni mafanikio makubwa sana kwa timu hizi. Kama mdhamini mkuu wa timu
hizi, Kilimanjaro Premium Lager imeona umuhimu wa kuziunga mkono klabu hizi
katika jitihada zake kutuletea tena fainali yenye burudani.” Alisema.
Aliongeza kuwa
Kombe la Kagame ndio mashindano makubwa zaidi ya yanayohusisha vilabu katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ni fursa zuri kwa wachezaji wetu
kuonyesha vipaji vyao kwa kushindana na wachezaji bora zaidi wa soka katika
ukanda huu na pia ni fursa nyingine kwa wanaohusika na timu ya taifa kuweza
kuchagua wachezaji.
“Ushirikiano kati ya Kilimanjaro Premium Lager na klabu
hizi umejikita katika mambo yanayotuunganisha kama vile ushirikiano, umoja na
kujituma kufanya kilicho bora. Tunaendelea kutimiza wajibu wetu kwa klabu hizi
na tuko tayari kupeleka mpira wa Tanzania kwenye kilele cha mafanikio.”
Kaimu Meneja huyo
pia aliwasihi Simba na Yanga kuhakikisha wanaiwakilisha nchi vizuri katika
mashindano haya makubwa kikanda na kuwafanya Watanzania wajivunie klabu hizo
kwa kuiletea Tanzania ushindi wa kombe la Kagame kwa mara ya 11.
No comments