Nchi zaidi za Afrika zajiunga na APRM
Na
Mwandishi Wetu,Addis Ababa
Mataifa
zaidi ya Afrika yamesaini mkataba wa kujiunga na mchakato wa Afrika
Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) wakati wa kikao cha wakuu wa nchi za Umoja
wa Afrika (AU) zinazoshiriki katika tathmini ya APRM mjini hapa.
Mkutano
wa wakuu wa nchi zinazoshiriki APRM ulifanyika Jumamosi ikiwa ni siku moja
kabla ya kuanza kwa kikao cha wakuu wa nchi za AU ambapo Rais Jakaya Kikwete
aliongoza idadi ya Marais wa Afrika waliohudhuria mkutano huo wa APRM.
Nchi
mpya zilizosaini mkataba wa kukubali kukaguliwa kiutawala bora chini ya APRM ni
Niger, Cape Verde, Chad, Tunisia na Guinea ya Ikweta, hivyo kufikisha idadi ya
nchi 36 kati ya 54 wanachama wa AU walioamua kujiunga na mchakato wa APRM.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari na
Mawasiliano wa APRM Tanzania, Hassan Abbas, APRM huipa nchi fursa kuanzisha
taasisi yake ya ndani kwa lengo la kuwapa wananchi fursa ya mara kwa mara
kuitathmini nchi yao katika utawala bora, kisha tathmini hiyo kuhakikiwa na
wataalamu wengine kutoka nchi za Afrika kwa lengo la Afrika kama Bara na kila
nchi kujikosoa ili baadaye kujisahihisha.
Akizungumza
mjini Addis mara baada ya mkutano huo wa marais, Katibu Mtendaji wa APRM
Tanzania, RehemaTwalib alisema mkutano huo ulikuwa wa mafanikio na viongozi hao
walipitisha maazimio mengi ikiwemo kuiimarisha APRM ili kuwa taasisi kamili ya
Umoja waAfrika.
Rais
Kikwete aliunganana marais wengine akiwemo Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Waziri
Mkuu wa Ethiopia,Melesi Zenawi na Rais wa Uganda Yoweri Museveni katika mkutano
huo.
Mkutano
huo pamoja namambo mengine pia ulijadili taarifa ya utekeleza wa hali ya
utawala bora kwa nchiza Uganda, Burkina Faso na Algeria. Rais Abdulaziz
Bouteflika wa Algeria aliwakilishwa na Waziri Mkuu wan chi hiyo, Ahmed Ouyahia.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizojiunga mapema tu tangu mchakato huo
ulipoanzishwa mwaka 2003 kwa kusaini mkataba mwaka 2004, Bunge likauridhia
mwaka 2005 na tayari ripoti iliyosheheni maoni ya Watanzania kuhusu utawala
bora nchini imeshakamilika.
No comments