Rais Kikwete ahudhuria mkutano wa APRM
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja
na viongozi wengine wanchi za Afrika
wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 19 wa wakuu wan chi za umoja wa Afrika(AU)
jijini Addis Ababa Ethiopia leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
Na Mwandishi Wetu, Addis Ababa
RAIS Jakaya Kikwete wa Tanzania
amekuwa miongoni mwa Marais na viongozi wakuu wa Serikali mbalimbali za Afrika
waliohudhuria mkutano wa wakuu wa nchi zinazoshiriki katika Mpango wa Afrika
Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).
Rais Kikwete aliungana na marais
wengine akiwemo Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Melesi
Zenawi na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine
ulijadili taarifa ya utekeleza wa hali ya utawala bora kwa nchi za Uganda,
Burkina Faso na Algeria. Rais Abdulaziz Bouteflika wa Algeria aliwakilishwa na
Waziri Mkuu wan chi hiyo, Ahmed Ouyahia.
Akizungumza mjini Addis mara baada
ya mkutano huo wa marais, Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Rehema Twalib
alisema mkutano huo ulikuwa wa mafanikio na viongozi hao walipitisha maazimio
mengi ikiwemo kuiimarisha APRM ili kuwa taasisi kamili ya Umoja wa Afrika.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 32 za
Afrika zinazoshiriki katika mchakato wa APRM unaolenga kuzipa fursa nchi za
Afrika kujitathmini Kiutawala Bora kwa kuwapa nafasi wananchi wao na wataalamu
wao wa ndani kutoa maoni yao. Mchakato huu ni endelevu na hurudiwa kila baada
ya miaka minne.
Taarifa kutoka mjini Addis zinaonesha
kuwa nchi nyingine tano zimetangaza kujiunga na taasisi ya APRM kupitia mkutano
huo uliofanyika jana (Jumamosi Julai 14, 2012).
No comments