Wagonjwa 15 wenye matatizo ya mishipa ya damu kutanuka na kuchanika kufanyiwa upasuaji
Madaktari bingwa wa upasuji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Cardio Start International la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu mgonjwa ambaye mishipa yake ya damu imeziba wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Maalumu, Dar es Salaam.
WAGONJWA 15 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya kifua kutanuka au kuchanika (Ascending Aortic Aneurysm and Dissection), wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa moyo na watalaamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Cardio Start International la nchini Marekani.
Upasuaji huo unafanyika katika kambi maalumu ya siku tano inayofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Benjamini alisema wataalamu wa Cardio Start International walianza na kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo ambayo yatatusaidia kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wao.
“Katika kambi hii tutawafanyia upasuaji wagonjwa wenye matatizo ya mishipa ya damu mikubwa kutanuka au kuchanika, tutazibua mishipa ya moyo iliyoziba na kuziba milango ya moyo inayovuja,” alisema Dkt. Alex.
Madaktari bingwa wa upasuji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Cardio Start International la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu mgonjwa ambaye mishipa yake ya damu imeziba wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanyika katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Chake Chake kisiwani Pemba kwa ajili ya kwenda kufanya mkutano wa kampeni katika eneo la Kinyasi, wilayani Wete leo Oktiba 8, 2025.
DkT. Nchimbi anafanya mkutano huo kwa ajili ya kumuombea kura Mgombea urais wa chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan, Mgombea urais wa Zanzibar, DkT.Hussein Ali Mwinyi, wagombea wa ubunge, uwakilishi pamoja na udiwani.
No comments