Header Ads

ad

Breaking News

DKT.NCHIMBI AWASILI JIJINI ARUSHA KUENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amewasili mkoani Arusha leo Ijumaa Septemba 12,2025 na kuendelea na mikutano yake ya kampeni akitokea Mkoa wa Katavi.

Mara baada ya kuwasili jijini humo, Balozi Dkt.Nchimbi ataelekea wilayani Longido, Jimbo la Longido, ambako atawahutubia wananchi wa jimbo hilo na kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya mkoa huo, akiwemo mgombea ubunge wa Jimbo la Longido, Dkt Steven Lemomo Kiruswa na madiwani.

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Aidha, amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025






No comments