Friday, September 12, 2025

DKT.NCHIMBI AHUTUBIA NA KUZINDUA KAMPENI ZA JIMBO LA ARUSHA MJINI

Na Mwandishi Wetu, Arusha

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, akiwahutubia Wananchi kwenye Mkutano wake wa Kampeni leo Ijumaa Septemba 12,2025 katika Uwanja wa Soweto, jijini Arusha.

Akiwa katika  mkutano huo Dkt Nchimbi pia alipata wasaa wa kuwanadi wagombea Ubunge  wa mkoa huo, akiwemo Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul  Christian Makonda pamoja na madiwani.

Aidha, Dkt. Nchimbi pia aliongoza uzinduzi wa mikutano ya kampeni kwa Jimbo la Arusha Mjini mbele ya Wananchi waliofika kumsikiliza.

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Mgombea mwenza huyo amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.

Dkt. Nchimbi siku ya leo ameanza kufanya mikutano ya kampeni mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa kuanzia Arusha ambapo amefanya mikutano mitatu akianzia Longido, Arumeru Magharibi na kumalizia Arusha Mjini huku umati wa wananchi ukitoa ahadi ifikapo siku ya uchaguzi wao wanatiki kwa wagombea wa chama hicho.















No comments:

Post a Comment