Saturday, September 13, 2025

DTK.NCHIMBI AANZA KUSAKA KURA KANDA YA KASKAZINI

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akiwasalimia Wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai,akiendelea na mikutano yake ya Kampeni leo Jumamosi Septemba 13,2025 mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt. Nchimbi ambae ni mgombea mwenza wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,pia alitumia nafasi hiyo kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai Ndugu Saashisha Mafuwe pamoja Diwani.

Dkt.Nchimbi ambae ameingia Kanda ya Kaskazini,akianzia mikutano yake ya Kampeni Mkoani Arusha na ameingia mkoa wa Kilimanjaro kusaka kura za ushindi wa Kishindo za Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2025-2030, ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Ngombea mwenza huyo amekuwa akitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.







No comments:

Post a Comment