Friday, September 12, 2025

DKT NCHIMBI ANADI SERA ZA CCM LONGIDO

Na Mwandishi Wetu, Longid

MGOMBEA Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John  Nchimbi, amewahutubia Wananchi wa Longido kwenye mkutano mdogo wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Polisi, leo Ijumaa Septemba 12,2025.

Mara baada ya kuwasili eneo la Mkutano, Balozi Dkt.Nchimbi alikaribishwa kwa kuvalishwa vazi la heshima la Kichifu kutoka kwa Viongozi wakuu wa kimila wa Kabila la Kimasai  (Malaigwanani).

Akiwa kwenye mkutano huo, Balozi Dkt.Nchimbi alipata wasaa pia wa  kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya  Mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Longido, Dkt.Steven Lemomo Kiruswa pamoja na madiwani.

Dkt. Nchimbi ameendelea kuinadi Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa Maendeleo katika miaka mitano ijayo.

Aidha, amekuwa akitumia  nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM,Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan, wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025.








No comments:

Post a Comment