Jumaa awashukia wanaohama CCM
Na Omary Mngindo, MlandiziMGOMBEA nafasi ya Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humoud Jumaa, amesikitishwa kwa kitendo cha wanachama wenzake kukihama chama hicho, kisa kushindwa kwenye uchaguzi.
Aidha, amesema kuwa kuna haja kwa uongozi wa chama hicho kuweka utaratibu utaowadhibiti wanaSiasa wa aina hiyo, ambapo kwa atayekihama wekewe masharti magumu ya kurejea.
Jumaa alitoa kauli hiyo muda mfupi kabla ya kwenda kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo kwenye Ofisi za Tume ya uchaguzi, katika Jengo la Halmashauri lililopo Kitongoji cha Kisabi Kata ya Mtongani.
"Inashangaza kuona mwanaCCM akishindwa katika uchaguzi kuanzia kura za maoni, uteuzi au kwenye uchaguzi anakihama chama anajiunga vyama vingine, inashangaza sana tutapeleka mapendekezo kwa viongozi ili watu wa aina hii wasipokelewe tena," alisema Jumaa.
Aliongeza kuwa ndani ya chama hicho kuna michakato mbalimbali na nafasi tofauti za uongozi, huku akiongeza kuwa mwaka 2020 alishinda kura za maoni lakini vikao ngazi za juu vikamchuja akateuliwa mwingine alitulia, akaendelea kukipigania chama hicho.
"Nilishinda kura za maoni, nikakatwa na vikao ngazi za juu nikatulia ikatokea nafasi ya UNEC nikagombea nikashinda, hiyo ni sistimu ya chama chetu ukishindwa nafasi moja una nafasi ya kugombea nyingine na si kuhama chama, huko nako ukishindwa utakimbilia wapi?", alisema Mteule huyo.
Akizungumzia matarajio yake pindi akichaguliwa kuwa Mbunge Jumaa alisema kuwa anakuja kivingine, huku akieleza kuwa kukaa kwake nje kwa miaka mitano kuna mambo amejifunza, huku akiwaambia wanaKibaha Vijijini wajiandae kupokea maendeleo sekta zote.
"Kukaa nje ya Ubunge kwa miaka mitano kuna mambo mengi nimejifunza, wanaKibaha Vijiji mtarajie maendeleo makubwa katika sekta mbalimbali, niwaombe wampatie kura za kutosha mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu, Mimi na Madiwani wote wa CCM," alimalizia Mteule huyo ambae wananchi wanaimani nae kubwa.
Aidha, amesema kuwa kuna haja kwa uongozi wa chama hicho kuweka utaratibu utaowadhibiti wanaSiasa wa aina hiyo, ambapo kwa atayekihama wekewe masharti magumu ya kurejea.
Jumaa alitoa kauli hiyo muda mfupi kabla ya kwenda kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo kwenye Ofisi za Tume ya uchaguzi, katika Jengo la Halmashauri lililopo Kitongoji cha Kisabi Kata ya Mtongani.
"Inashangaza kuona mwanaCCM akishindwa katika uchaguzi kuanzia kura za maoni, uteuzi au kwenye uchaguzi anakihama chama anajiunga vyama vingine, inashangaza sana tutapeleka mapendekezo kwa viongozi ili watu wa aina hii wasipokelewe tena," alisema Jumaa.
Aliongeza kuwa ndani ya chama hicho kuna michakato mbalimbali na nafasi tofauti za uongozi, huku akiongeza kuwa mwaka 2020 alishinda kura za maoni lakini vikao ngazi za juu vikamchuja akateuliwa mwingine alitulia, akaendelea kukipigania chama hicho.
Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humoud Jumaa, akitembea pamoja na viongozi mbalimbali.

No comments