Header Ads

ad

Breaking News

Wazazi wa wanafunzi Innovate wapongeza mafunzo

Na Omary Mngindo, Mlandizi

WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma katika Shule Awali na Msingi ya Innovate iliyopo Kitongoji cha Kibwende, Kata ya Mlandizi Kibaha Vijijini mkoani Pwani, wameushukuru uongozi wa shule hiyo kwa kuwapeleka wanafunzi kujifunza wilayani Bagamoyo.

Wakizungumza shuleni hapo walipokwenda kuchukua taarifa za wanafunzi wao baada ya kufunga shule, wazazi hao walisema hatua hiyo imeleta faraja kwa watoto wao.

Wakijitambulisha kwa majina ya Rehema Adam, mzazi wa Omary Said, alisema ziara hiyo ya kujifunza mambo mbalimbali imemwongezea kitu mtoto wake, alijionea nyumba za kale na kutembelea vivutio mbalimbali.

"Alinielezea mambo mengi, kiukweli ziara imempatia kitu mtoto wangu, ameniambia amejionea maeneo waliyopita watumwa, na kushuhudia wanyama wanaotambaa, wakiwemo nyoka, kobe na wengine," almesema Rehema.


Naye, Letisia Charles, mzazi wa Blandina Ngassa amesema mtoto wake aliifurahia safari hiyo, ambayo imemwongezea kitu mwanafunzi huyo.

"Alipofika tu nyumbani alianza kunielezea safari hiyo, ikiwemo kujionea Bahari ya Hindi, kupanda ngamia, na nyumba za kale, ikiwa ni moja ya vivutio vinavyowaleta watalii nchini," amesema mzazi huyo.

Badru Swai na Newaho Mkisi walisema kuwa, wanaunga mkono juhudi za uongozi wa shule chini ya Mkurugenzi George Ndaki, Mwalimu Mkuu Sir Side na wasaidizi wake ambao kwa pamoja wanajitahidi kuwafundisha watoto wao.

Mkurugenzi wa shule hiyo, Ndaki ameeleza namna wanafunzi walivyoonesha uwezo wa kujibu maswali katika moja ya maeneo waliyotembelea, ikiwemo kutambua baadhi ya mambo ambayo wamejifunza katika safari hiyo.

"Nianze kuwashukuru wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma shuleni hapa, kiukweli wamenufaika na safari ya kujifunza, wameshuhudia vitu vingi ikiwemo kuwaona ngamia, kuogelea katika Bahari ya Hindi na vitu vingine tofauti" amemalizia Ndaki.




No comments