Header Ads

ad

Breaking News

KAMPUNI KUBWA ZA MADINI ZASAINI MKATABA WA KUUZIA DHAHABU BENKI KUU TANZANIA(BOT)

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde

▪️Rais Samia apongezwa kwa maono

▪️Kampuni za GGM,Shanta na Buckreef kuuza Dhahabu kwa BOT,GGR kusafirisha dhahabu.

▪️BOT yanunua tabi 5 ya dhahabu 

▪️Waziri Mavunde apongezwa kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Madini

▪️Tanzania kuingia 10 bora kwa nchi zenye hifadhi kubwa ya Dhahabu Afrika

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Benki ya Tanzania(BOT) leo imesaini mikataba na Kampuni za Uchimbaji Madini za Geita Gold Mine(GGM),Buckreef Gold Ltd na Shanta Ltd juu kampuni hizo kuiuzia BOT kiasi kisichopungua asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa kama ambayo imeelezwa kwenye kifungu cha 59 cha Sheria ya Madini,Sura ya 123.

Hafla hiyo ya utiaji saini mikataba ya uuzwaji wa dhahabu imefanyika leo tarehe 16.06.2025 Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Madini, MAnthony Mavunde.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mwigulu Nchemba amempongez, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wenye maono na ambao umechochea kukua kwa hifadhi ya dhahabu ya BOT hali ambayo itasaidia kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba

“Serikali kupitia Wizara ya Fedha itaendelea kuhakikisha inaiwezesha Benki kuu katika manunuzi ya dhahabu ili kuongeza akiba ya nchi ya 𝙢𝙤𝙣𝙚𝙩𝙖𝙧𝙮 𝙜𝙤𝙡𝙙.

Nampongeza Waziri Mavunde kwa usimamizi mzuri wa sekta ya madini mpaka kufikia hatua hii,naamini kwa miaka michache ijayo nchi yetu itakuwa miongoni mwa nchi zenye akiba kubwa ya hifadhi ya dhahabu kupitia Benki Kuu,”alisema Mwigulu.

Naye, Waziri wa Madini, Mavunde amezipongeza Kampuni zote za uchimbaji na usafishaji madini kwa kusaini mikataba hiyo ambayo ina matokeo makubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania na kuchochea uongezaji thamani madini nchini.

Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Emmanuel Tutuba

Mavunde aliongeza kuwa hatua ya ununuzi wa dhahabu wa BOT kupitia wachimbaji wadogo na wakubwa utaiweka Tanzania kwenye ramani ya Afrika kuwa miongoni mwa nchi 10 zenye hifadhi kubwa ya dhahabu kupitia Benki Kuu.

Akitoa taarifa ya awali Gavana wa Benki Kuu, Emmanuel Tutuba amesema hatua hii ya ununuzi wa dhahabu kupitia BOT utasaidia kuimarisha Uchumi na Shilingi ya Tanzania na kwamba imejipanga kuikuza hifadhi hii ya dhahabu kwa kuendelea na ununuzi kila mwaka ili kufanikisha azma ya Serikali ya kuwa na hifadhi ya dhahabu itakayoihakikishia Tanzania uchumi imara.

Gavana Tutuba  ameongeza kwamba mpaka sasa BOT imeshanunua Tani 5.02 huku lengo likiwa kununua Tani 6 za dhahabu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo malipo yote yamefanyika ndani ya masaa 24.









No comments