Header Ads

ad

Breaking News

Rais Dkt.Mwinyi akutana na viongozi Kamati ya Amani

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na viongozi wa Kamati ya Amani ya viongozi wa dini Zanzibar


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Kamati ya Amani ya viongozi wa dini Zanzibar kujadili mustakabali wa amani kuelekea uchaguzi mkuu wa  Oktoba mwaka huu.


Dkt,Mwinyi ameihakikishia kamati hiyo kuwa serikali inafanya kila juhudi kuhakikisha mifumo yote ya uchaguzi inafanya kazi kwa uhuru, amani na uwazi wakati wa  kampeni, upigaji kura na matokeo ya uchaguzi kwa dhamira ya kudumisha amani iliopo kwa maslahi ya nchi.

Rais Dkt, Mwinyi ameishauri Kamati Hiyo kuwakutanisha wanasiasa kufanya mjadala wa pamoja kuzungumzia umuhimu wa amani ya nchi pamoja na kudhibiti viashiria vya Uvunjifu wa Amani kabla na Baada ya Uchaguzi .

Aidha ameahidi Serikali Kuendelea kushirikiana na kamati hiyo ambayo imekuwa ikifanya kazi muhimu ya kuhubiri amani tangu ilipoasisiwa mwaka 2005.

Rais Dkt.Mwinyi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar amesema CCM ipo tayari kukaa pamoja na vyama vyengine vya siasa kujadili amani ya nchi.

Rais Dkt, Mwinyi ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wanasiasa kuzungumza uhalisia kuhusiana na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuepusha taharuki ndani ya jamii.

Rais Dkt, Mwinyi amesema mshikamano wa wananchi na amani ni tunu muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi.

Naye, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab amesema mkakati wa kamati hiyo ni kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa ya amani wakati wa uchaguzi, na baada ya uchaguzi na wananchi waingie katika uchaguzi kwa uwazi, upendo na furaha.

Kamati hiyo imemkabidhi Rais Dkt, Mwinyi Kitabu Maalum cha Muongozo wa Viongozi wa Dini Kuhusu Uchaguzi.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab



No comments