Header Ads

ad

Breaking News

CHARLES HILARY KUAGWA MAPINDUZI SQUARE ZANZIBAR

Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utumishi wa Ofisi ya Rais, Ikulu, Rajab Ali Ramadhan, akiambatana na maafisa mbalimbali wa Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, amekagua eneo la Mapinduzi Square, Kisonge, Mkoa wa Mjini Magharibi, kwa ajili ya maandalizi ya shughuli ya kumuaga Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Marehemu Charles Martin Hilary, aliyefariki dunia Mei 11,2025 jijini Dar es Salaam.

Kutokana na mabadiliko ya ratiba, Marehemu Charles Martin Hilary ataagwa Mei 14, 2025 katika Viwanja vya Mapinduzi Square (Kisonge), badala ya ukumbi wa Idris-Abdulwakil.

Mwili wa Marehemu Charles Martin Hilary utapokelewa kesho, Mei 13,2025, saa 11:30 jioni katika Bandari ya Malindi, Zanzibar na kuzikwa Mei 14,2025 saa 10 jioni katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi.







No comments