Header Ads

ad

Breaking News

Mchengerwa aelezea wagombea waliokatwa

Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika semina iliyowahusisha wahariri wa vyombo vya habari leo Jumanne Novemba 12,2024

Na Mwandishi Wetu

WAGOMBEA wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao wamekatwa kutokana na kasofro mbalimbali kwenye fomu zao, bado wana nafasi ya kukata rufaa.

Rufaa zinazokatwa ngazi ya Wilaya zinapaswa kukatwa na wagombea wenyewe si vyama vya siasa, hivyo wanaweza kutumia muda uliobaki kabla ya mwisho wa rufaa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, alitoa kauli hiyo leo Novemba 12,2024 jijini Dar es Salaam  kwenye semina ya wahariri wa vyombo vya habari iliyohusu Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Amesema muda wa kukata rufaa ulianza Novemba 10 hadi leo na kuwataka wagombea, kutumia fursa hiyo, badala ya kukaa nyumbani wakilalamika na kuviacha vyama vya siasa vipiganie rufaa zao.

“Rufaa inapaswa kukatwa na mgombea mwenyewe si chama cha siasa, wale wanaoona hawajatendewa haki bado wana muda wa kukata rufaa,” alisema.

Ameeleza kuwa, uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Novemba 27, 2024 utashirikisha vyama 19.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa TAMISEMI, mihayo Kadete, alisema ujasiriamali ni kazi halali inayotambulika kiserikali.

“Si sawa sawa kuwaengua wagombea kwenye uchaguzi huo kwa sababu ya kigezo cha kujaza kazi ujasiriamali ambayo ni kazi halali kiserikali, mtu aliyeenguliwa anapaswa kukata rufaa,” alisema.

Aliongeza kuwa, mgombea ambaye hajajiandikisha kupiga kura katika eneo lake ni moja ya sababu ya kukosa sifa ya kugombea katika uchaguzi huo.

Semina hiyo iliyohusu masuala ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa iliandaliwa na TAMISEMI.


Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika semina iliyowahusisha wahariri wa vyombo vya habari

Mkuu wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mhandisi Andrew Kisaka akizunngumzia kutoa haki ya utangazaji kwa vyama vyote wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

No comments