Header Ads

ad

Breaking News

RIDHIWANI AONYA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KUTUMIANA NYARAKA ZA SERIKALI

NAIBU Waziri wa Nchi Menejimenti ya  Utumishi Wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, ameonya matumizi ya mitandao ya kijamii kutumiana nyaraka za serikali.

Ridhiwani ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Jennyjerry Ntate, Bungeni Dodoma leo.

Naibu Waziori amewakumbusha wabunge na wananchi kuwa, mawasiliano serikalini yanasimamiwa na sheria na kanuni hivyo, ni muhimu kwa wananchi kuzingatia taratibu hizo ili sheria zisiwabane na kuleta taharuki isiyokuwa ya msingi. 

Kufuatia kauli hiyo ya Serikali, Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda, akataka kujua ni jinsi gani serikali imejipanga kwenye ujenzi wa mifumo ukizingatia teknolojia ndiyo inakwenda kwa haraka sana. 

Akijibu swali hilo , Naibu Waziri Kikwete ameeleza kuwa wazi kumeendelea kujenga mifumo mbalimbali ya tehama na uwepo wa sheria Namba 10/2019 umewezesha serikali kuwa na uhalali wa uundaji wa mifumo hiyo na hadi sasa mifumo mbalimbali imejengwa kusaidia mawasiliano serikalini na kurahisisha uchapaji kazi.






No comments