TFF YATAKA WALIOVURUNDA KUPANGA RATIBA YA LIGI KUU BARA 2017-18 WACHUKULIWE HATUA
![]() |
Kaimu Katibu Mkuu TFF, Kidao Wilfred (katikati), Salum Madadi (kulia) na Alfred Lucas, Msemaji wa shirikisho hilo. |
Na.Alex Sonna
Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini TFF chini ya Rais Mpya Wales Karia,limepanga kuwachukulia hatua
ya kinidhamu viongozi wa bodi ya Ligi wote ambao walihusika na upangaji
wa ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa mwaka 2017-18
wakiongozwa na Bonifance Wambura ambaye ndio mhusika Mkuu katika swala
la ratiba.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,Wilfred Kidao amesema kuwa uongozi wa shirikisho hilo umeamua kuchukua jukumu hilo baada ya kubaini wataalamu hao wameshindwa kupanga vizuri ratiba ya ligi hivyo Rais wa TFF,Wallace Karia ametoa agizo kwa mtendaji wa bodi ya ligi achukue Jukumu la kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na hatua hiyo.
“Nimeagizwa na rais nimwandikie
barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi ili aweze kuwachukulia hatua
viongozi wa bodi hiyo waliohusika na kupanga ratiba hii pamoja na kwamba
walikuwa na kalenda lakini bado wamekosea,” alisema Kidao.
Kidao amesema kuwa ratiba hiyo
ilipangwa kwa makosa makubwa hivyo kupelekea kuwa na dosari mapema
baada ya kuchezwa mechi moja tu ya Ligi Tayari imeanza kupanguliwa
kutokana na kuingiliana na Kalenda ya FIFA hivyo kusababisha Ligi Kuu
Kusimama kwa muda kupisha mechi ya Kirafiki kati ya Tanzania na Botswana
inayotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Uhuru jijini
Dar es salaam.
Aidha amesema kuwa TFF imetoa agizo kwa uongozi wa bodi ya
ligi kuiangalia upya ratiba hiyo ya ligi na pia imeteua kikosi cha watu
wa nne ambacho kitakuwa na jukumu la kuifanyia marekebisho ya msingi
ratiba hiyo ambayo hayataleta athari katika ligi hiyo.
Kwa kumalizia Kidao amesema kuwa
kamati aliyeiteua inatakiwa kufika mpaka siku ya Jumapili iwe
imeshampelekea ratiba yote na kwa sasa Bodi ya Ligi haitaweza kutoa
ratiba ya Ligi bila kupitiwa na Katibu Mkuu wa TFF hivyo Mtendaji Mkuu
wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la
kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.
No comments