TAARIFA KUTOKA BENKI KUU YA TANZANIA KUHUSU KUBADILISHA FEDHA

Benki Kuu ya Tanzania inapenda
kuutaarifu umma kupuuza taarifa zinazozunguka katika mitandao ya kijamii
kwamba kutakuwa na ‘mabadilisho ya fedha zote za zamani kuanzia tarehe
04/09/2017 hadi tarehe 01/12/2017’.
Taarifa hizo ni za uongo na
hazijatolewa na Benki Kuu ya Tanzania. Wananchi mnaombwa kuendelea na
taratibu zenu za kawaida za kufanya miamala yenu mbalimbali kwa kutumia
fedha zetu kama kawaida.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
inawaasa watumiaji wa mitandao ya kijamii kutumia vizuri nyenzo hiyo ya
kupashana habari na kuacha kuzusha uongo ambao unaleta usumbufu usio wa
lazima kwa wananchi.
Imetolewa na:
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Barua pepe: info@bot.go.tz
Simu: +255 22 2233167
No comments