CHIRWA, KASEKE WASHINDA HUKUMU YAO MSUVA AKUTWA NA HATIA SASA TFF KUMPA BARUA

Na Alex Sonna
Hatimaye wachezaji watatu wa
Yanga ambao walisimamishwa na bodi ya Ligi leo Kamati ya nidhamu ya TFF
imewaachia huru Obrey Chirwa na Deus Kaseke huku Simon Msuva akipewa
onyo kwa njia ya maandishi baada ya kamati hiyo kubaini kuwa wachezaji
hao hawakupaswa kupewa adhabu ya kusimamishwa.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya
nidhamu ya TFF,Peter Hella alisema kuwa kamati hiyo baada ya kupokea
uteteza kwa wachezaji hao na kupata ushahidi wa picha ya mnato imebaini
ni mchezaji pekee Simon Msuva ndiye aliyekutwa na makosa baada ya
kumuangusha mwamuzi wa mechi husika kutokana na madai ya Yanga kunyimwa
penalti.
Aidha amesema kuwa kamati hiyo
itamuandikia barua ya onyo kali mchezaji Simon Msuva kwa kitendo chake
ambacho alikifanya licha ya kuwa tayari alishaanza kutumikia adhabu ya
kosa hilo ikiwemo kukosa kucheza baadhi ya mechi za Yanga kipindi
ambacho timu hiyo ilishiriki michuano ya SportPesa.
Wachezaji hao kwa pamoja wakati wanaitumikia timu ya Yanga
msimu uliopita walisimamishwa na kamati ya masaa 72 baada ya kuonekana
wamemuangusha mwamuzi katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara
uliowakutanisha Yanga na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba mjini
Mwanza.
Mchezo huu Mbao FC walishinda
kwa goli 1-0 lililofungwa na Habibu Haji baada ya makosa ya beki wa
Yanga Vicent Andrew licha ya Simon Msuva kuhamia nchini Morocco huku
Deus Kaseke akiwa amehamia katika timu ya Singida United ya Mkoani
Singida.
www.fullshangweblog.com
No comments