Mbunge Aysharose alipongeza kanisa kwa kuwaelimisha vijana 490 umuhimu wa kulipa kodi
Vijana Kanisa Katoliki Jimbo la Singida waliohudhuria
kongamano la wiki moja, lililofanyika kwenye jukwaa la Askofu Mabula mjini
Singida.
|
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida Aysharose
Mattembe akitoa nasaha zake kwenye kongamano la vijana wa kanisa katoliki jimbo
la Singida.
|
Na Nathaniel Limu
Mbuge Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Aysharose
Mattembe (CCM), amelipongeza Kanisa la Romani Katoliki (RC), Jimbo la Singida kwa
uamuzi wake wa kuwaelimisha vijana 490 umuhimu wa kulipa kodi.
Mattembe ametoa pongezi hizo wakati akizungumza kwenye
kongamano la vijana waumini wa kanisa hilo lililofanyika kwenye jukwaa la
askofu Mabula kwenye viwanja vya kanisa katoliki mjini hapa.
Amesema vijana wakiwezeshwa kutambua mapema umuhimu wa
kulipa kodi na manufaa yake, nchi itakuwa ya walipa kodi ambao watalipa kwa
hiyari yao bila kushurutishwa.
“Suala la kulipa kodi ni muhimu mno kwa maendeleo ya
nchi yo yote hapa duniani. Rais wetu Dkt Magufuli ameleta mageuzi makubwa
mno yanayohusu kulipa kodi. Anajua umuhimu wa kulipa kodi kwa sababu bila kodi
hakuna maendeleo. Baba Askofu, kitendo chenu cha kutoa elimu ya kodi kwa vijana
hawa mtakuwa mmemuunga mkono rais Magufuli na hongereni sana”, amesema
Mattembe.
Mbunge huyo amewataka vijana hao ambao wametoka wilaya
zote za mkoa wa Singida,wakawe mabalozi wazuri katika kueneza elimu ya kulipa
kodi kwa wenzao ambao hawakubahatika kuhudhuria kongamano hilo.
“Vijana wenzangu haya maendeleo makubwa
mnayoyaona ya barabara nzuri, vituo vya afya na visima vya maji na maengine
mengi, yote yanagharamiwa na fedha za kodi na si vinginevyo. Serikali ya awamu
ya tano inamtaka kila mtanzania mwenye sifa ya kulipa kodi alipe, tena kwa
wakati bila ya kushurutishwa”, amesisitiza.
Aidha amaewataka vijana wote mkoani hapa wenye sifa ya
kufanya kazi, wajiunge kwenye vikundi vya ujasiariamali pamoja na vile vya
kilimo cha biashara, ili waweze kujiletea maendeleo na kujikomboa kiuchumi.
“Faida za kujinga kwenye vikundi vilivyosajiliwa ni
nyingi ikiwemo ya kupata mikopo kwa masharti nafuu kutoka taasisi za kifedha.
Tunayo maeneo ya kutosha kwa ajili ya ufugaji nyuki. Mazao ya nyuki yana soko
kubwa ndani na nje ya nchi. Anzisheni vikundi vya ufugaji nyuki mtaharakisha
kujikomboa kiuchumi. Nina uhakika serikali ya mkoa na ofisi yangu tutawasaidia
ili muweze kufikia malengo yenu”, amesema.
Mattembe ameahidi kuchangia mizinga ya kisasa ya
kutosha kwa vijana watakaojiunga katika vikundi huku akiungwa mkono na Katibu
wa Jumuiya ya Wanawake (CCM) Manispaa ya Singida Magreth Malecela ambaye
ameahidi kuchangia mizinga mitano ya kisasa.
Awali Baba askofu wa jimbo la Singida Edward Mapunda
amesema vijana hao pia wamepewa elimu juu ya ujasiriamali, kilimo cha biashara
na maadili mema.
Aidha, amesema kongamano hilo ambalo linafanyika kila
mwaka mara moja, linatarajia kupanua wigo kwa kupata wawezeshaji wa fani
mbalimbai kutoka nje ya mkoa.
No comments