MBAO FC YAPATA UDHAMINI WA GF TRUCKS, WAPEWA MILIONI 70 NA BASI LA SAFARI ZAO

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Mbao FC ya Mwanza iliyo katika msimu wake wa pili tangu ipande Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, leo imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na kampuni ya uagizaji wa magari ya mizigo GF Trucks & Equpments wenye thamani ya Sh. Milioni 140.
Akizungumza kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ofisa Masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala amesema kwamba ndani ya mkataba huo wataipatia klabu hiyo basi lenye thamani ya Sh. Milioni 70 pamoja na fedha taslimu Sh. Milioni 70.
Pia tunawapongeza Mbao FC kwa mwanzo mzuri wa Ligi kwa
kuwafunga Kagera Sugar,” amesema Bundala.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Solly Zephania Njashi ameishukuru kampuni ya GF kwa kuingia nao mkataba huo na basi hilo litawasaidia katika safari mbalimbali kipindi hiki cha Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
“Tunawashukuru GF kwa kukubali kutudhamini, fedha hizi pamoja na basi vitatusaidia kwenye klabu yetu, hasa basi litatusaidia sana katika safari za mikoani ambazo tutaenda kucheza mechi za Ligi Kuu," amesema Njashi.
Huo unakuwa udhamini wa pili kwa washindi hao wa pili wa Azam Sports Federation Cup, baada ya mwaka jana kupata udhamini wa Hawaii Products Supplies, watengenezaji wa maziwa ya Cowbell wenye thamani ya sh. milioni 50 kwa msimu.
No comments