Header Ads

ad

Breaking News

Barcelona yamsajili Ousmane Dembele kwa pauni milioni 135.5

                                                              Ousmanne Dembele. (Getty Images
 
 
BARCELONA, Hispania
Barcelona wamekamilisha usajili wa mshambualiji wa Borrusia Dortmund, Ousmane Dembele kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 135.5.


Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 ametia saini kandarasi ya miaka mitano katika Uwanja wa Nou Camp akiwa na Rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu, jana Jumatatu.

Kandarasi hiyo ni ya pili kwa thamani baada ya ile ya hivi karibuni ya Neymara aliyesajiliwa na PSG ya Ufaransa kwa kitita cha pauni milioni 200.

Dembele: Nafurahia sana kujiunga na Barca .
''Imekuwa ndoto yangu tangu nikiwa mdogo kuichezea Barca na sasa nimewasili''.

''Ndiyo klabu bora duniani ilio na wachezaji bora duniani''.

Mara ya mwisho kwa Dembele kuichezea Dortmund ni wakati wa kombe la Supercup mnamo Agosti 5 mwaka huu.

Klabu hiyo ya Bundesliga ilikataa ombi la Barca mapema mwezi Agosti , huku mchezaji huyo akiwa amepewa marufuku kwa kukosa mazoezi.

No comments