MAJAMBAZI YAVAMIA DRFA, YAMPORA KATIBU NA WAFANYAKAZI WENGINE, YALIKUWA YANADAI KUNA SH MILIONI 150, YAPEWE
Watu
wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamevamia kwenye ofisi za Chama cha
Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwapora baadhi ya wafanyakazi
akiwemo katibu mkuu wa chama hicho, Kanuti Daudi.
Watu
hao walivamia ofisi za DRFA leo asubuhi na kufanya uboraji huo huku
wakiagiza kupewa Sh milioni 150 zilizokuwa ndani ya ofisi za DRFA.
Katibu huyo amesema, kabla ya kufika, wenzake walionyeshwa silaha kama alivyoelezwa lakini yeye hakuiona.
"Wenzangu wanasema awali walionyesha silaha, mimi sikuiona baada ya kufika ila niliona mmoja akiwa na pingu."
Kanuti amesema baada ya kufika walimtaka kuingia kupanda juu, huko alikuta wafanyakazi wenzake wakiwa wamefungwa.
“Kufika
juu nikawakuta wenzangu wakiwa wamefungwa. Nikajumuishwa na kutakiwa
kutoa fedha Sh milioni 150 jambo ambalo lilinishangaza, nikawaambia
ntazitoa wapi.
“Wakaanza
kunisachi na kuchukua ufunguo uliokuwa mfukoni mwangu pamoja na fedha
kama Sh lakini mbili hivi. Tayari walikuwa wamewapokonya fedha baadhi ya
wafanyakazi wenzangu,” alisema.
“Baada
ya kuona hatuna kitu walichokuwa wanakitaka, walifanya uporaji huo wa
fedha kwetu pamoja na vifaa kama laptop halafu wakaondoka zao.
“Wana usalama walikuja baadaye sana, maana jamaa walikuwa wameishaondoka na wasamalia wema walikuwa tayari wametufungua.”
kwa hisani ya www.salehjembe.blogspot.com
No comments