Viongozi wa Afrika wakemewa na kuitwa 'Watalii wa kiafya'
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari
akishuka ndege baada ya kurejea nchini mwake mwezi huu wa Agosti baada
ya kuwa London, Uingereza kwa likizo ya siku 100 ya matibabu
|
Waziri mmoja nchini Afrika Kusini, amewakosoa vikali viongozi wa Bara Afrika ambao wanakwenda ng`ambo kutafuta matibabu.
Rais Robert Mugabe, ambaye mara kwa mara anapokea matibabu nchini Singapore, alikuwa ameondoka kutoka katika, mkutano huo unaohudhuriwa na mawaziri wa afya, ndipo Dkt Motsoaledi, alipotoa matamshi hayo.
Msemaji wa Bwana Mugabe, alikuwa amesema kuwa Daktari wa kibinafsi wa Rais Mugabe ''sio tu raia wa Zimbabwe," ni mtu mweusi.....Na ni mweusi, mweusi mweusi sana".
George Charamba, alsema hayo alipokuwa akihojiwa na gazeti la serikali ya Zimbabwe - The Herald, mwezi Mei mwaka huu, akisisitiza kuwa Rais Mugabe kamwe haipi kisogo sekta ya matibabu ya nchini hiyo.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari na mwenzake wa Angola José Eduardo dos Santos pia wamekosolewa vikali kwa kutafuta matibabu nje ya nchi mwaka huu.
"Sisi ndilo bara pekee duniani, ambalo viongozi wake wanatafuta matibabu matibabu katika mataifa ya kigeni yaliyoko nje ya bara hili, nje ya eneo letu. Inafaa tuaibikia hilo."
"Hii inaitwa utalii wa kiafya. Tunafaa kuboresha na kupigia debe kilicho chetu," aliongeza.
Dk. Motsoaledi pia ameyaomba mataifa ya Afrika kuongeza ufadhili wa kifedha kwa sekta ya matibabu.
Amepongezwa mno na raia nchini Afrika Kusini kwa kutumia hospitali za umma badala ya hospitali za kibinafsi.
Uchambuzi: Shingai Nyoka, BBC Victoria Falls, Zimbabwe
Orodha ya majina ya Marais wa Afrika waliokwenga ngambo kwa matibabu ni:- Robert Mugabe, Zimbabwe
- Muhammadu Buhari, Nigeria
- José Eduardo dos Santos, Angola
- Patrice Talon, Benin
- Abdelaziz Bouteflika, Algeria
Dkt Motsoaledi alikiri kuwa msimamo wake una utata, lakini aliamua kusema kindakindaki.
No comments