MULTICHOICE YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA DSTV! YAFYEKA BEI ZA VIFURUSHI VYOTE
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage
Chande akitangaza punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei
zitakazoanza kutumika rasi Septemba mosi 2017.
PANGA LA BEI LAFYEKA; DStv Premium kwa 8.15%, DStv Compact Plus kwa
11.02%, DStv Compact kwa 16.11%, DStv Family kwa 9.09% and DStv Access (Bomba)
kwa 4.88%
Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wote na watanzania kwa ujumla
wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya Multichoice Tanzania
imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa kufyeka bei za vifurushi vyake
vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake hususan
vile vya bei ya chini!
Habari hiyo njema
imetangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande,
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo
jijini Dar es Salaam ambapo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi
Septemba mosi 2017.
“Kumjali na kumsikiliza
mteja ni nguzo ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu
na wananchi kwa ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei,
tumechanganua kwa kina na tumeamua kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha
panga kwenye bei za vifurushi vyetu vyote!” alisema Maharage.
Akifafanua kuhusu punguzo
hilo, Maharage amesema kumekuwa na
punguzo la hadi asilimia 16, ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa
ahueni kubwa watumiaji wa DStv. Amezitaja bei mpya kuwa ni;
No comments