Conor McGregor kumfikia utajiri Cristiano Ronaldo
![]() |
Conor McGregor alipokutana na Cristiano Ronaldo |
DUBLIN, Ireland
Conor
McGregor amejipa matumaini ya kumpita kwa utajiri nyota wa Ureno na klabu ya
Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo katika jaridi la Forbes kufuatilia
pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather.

Bondia
huyo kutoka Dublin, pamoja na kuchapwa kwa Ko dhidi ya Mayweather anatarajia
kuingiza Zaidi ya dola milioni 77, kabla ya mkataba wake.
Ronaldo anaongoza
kwa utajiri kwa mwaka huu akiingiza Zaidi ya dola milioni 71, wakati McGregor juzi
alipigwa kwa Ko katika raundi ya 10 na bingwa wa masumbwi duniani Mayweather,
katika pambano lililofanyika Las Vegas.
Conor
McGregor alikutana na Cristiano Ronaldo mwaka jana na kumwambia anataka kumpita
kimpata katika listi ya utajiri.
McGregor atakuwa
nyuma ya Floyd Mayweather, wakati Forbes watakapotioa viwango vipya.
Ronaldo alimtembelea
bingwa huo UFC katika kambi yake ya mazoezi na bondia huyo alimweleza: 'Upo
katika nafasi ya kwanza katika listi ya matajiri kwenye jarida la Forbes, nilikuwa
namba 35 au namba Fulani hivi. Nitapanda. Inawezekana mwaka ujao nitakufikia.'
Ronaldo alimjibu: 'Sidhani kama utafika niliko.'
No comments