
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamis Kigwangallah
BAADA ya hivi karibuni dawa mpya ya kupambana na Virusi Vya UKimwi kugundulika na kuanza kutumika nchini Kenya, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini imefunguka, Uwazi lina habari kamili.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Nsachris Mwamwaja alisema wao kama wizara wanafurahi kusikia dawa imepatikana lakini akafafanua kwamba bado haijaingia Tanzania.
Aliongeza kuwa kama dawa hiyo itapitia taratibu zote za usajili, wizara haina tatizo wala kipingamizi.
“Kwa
sasa bado haijaingia Tanzania ila ikiingia tu tutawajuza wananchi ila
lazima ipitie taratibu zetu za usajili baada ya hapo ndipo ianze
kutumika,” alisema Mwamwaja.
www.mawingutz.blogspot.com
Baadhi
ya wananchi nchini walionesha kufurahishwa na ujio wa dawa hiyo nchini
Kenya wakiwa na imani kwamba zitaingia nchini na kusaidia waathirika wa
Ukimwi.CHA 8 ZA WASANII WA
TWANGA PEPETA WALIVYOJILIPUA JANA SIKU NA KUKAIDI AMRI YA BOSI WAO
A+
A-
Print
Email
Zaidi ya asilimia 80 ya wasanii wa Twanga Pepeta jana usiku walishiriki
onyesho la pamoja na bendi ya taarab ya Wakali Wao ndani ya ukumbi wa
Friends Corner Bar, Manzese jijini Dar es Salaam.
Wasanii hao walishiriki onyesho hilo kinyume na amri ya bosi wao Asha
Baraka ambaye hapo awali aliimbia Saluti5 kuwa haungi mkono wasanii hao
kushiriki show hiyo.
Asha Baraka akaenda mbali zaidi kwa kusema hata onyesho la Jumanne
iliyopita baina ya bendi hiyo mbili, lilifanyika bila idhini yake.
Kuelekea onyesho la jana, Asha Baraka akasema Twanga Pepeta haitashiriki
onyesho hilo ambalo hapo awali lilitangazwa kuwa litakuwa likifanyika
kila Jumanne ndani ya ukumbi huo wa Friends Corner huku likipewa jina la
“Usiku wa Wababe”.
Hata hivyo wasanii hao wa Twanga Pepeta walikuwa waungwana ambapo
walitii amri ya bosi wao ya kutopeleka bendi (African Stars – Twanga
Pepeta) na badala yake wakaenda kushiriki wao wenyewe bila jina la bendi
wala vyombo vya bendi – karoso nyimbo tu.
Naam nyimbo za Twanga Pepeta ndizo zilizosikika Friends Corner jana
usiku ambapo mwimbaji na rapa Khalid Chokoraa akasikika akitupia rap
inayosema: “hii ndondo, hii ndondo”.
Mwimbaji Kalala Jr naye akachombeza: “Wazee wa Kujilipua, wazee wa
kujitoa muhanga, kila Jumanne tuko hapa hata usiposikia tangazo, usiku
kibabe Ndondo Jazz Band na Wakali Wao”.
Kwa upande wake Ally Chocky yeye akasema: “Tukiwa kule ni Twanga Pepeta
lakini tukiwa hapa sisi ni Wakali Wao Jazz Band kwahiyo kila Jumanne
utakuwa unapata show ya Wakali Wao Modern Taradance na Wakali Wao Jazz
Band”.
Mmoja wa wasanii walioshiriki onyesho hilo akaiambia Saluti5 kuwa
hawakukaidi amri ya bosi wao maana wao wamekwenda kama wasanii wa Twanga
Pepeta na hawakwenda kama bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”.
“Tunamheshimu sana bosi wetu na kamwe hatuwezi kukiuka amri yake hasa
ukizingatia kuwa Jumanne bendi yetu huwa haifanyi kazi,” alisema msanii
huyo.
Hadi kamera ya Saluti5 inaondoka ukumbini hapo, sura za wasanii wakubwa
wa Twanga Pepeta ambazo hazikuonekana jukwaani ni Luizer Mbutu, Hajj BSS
na God Kanuti, lakini mastaa wengine wote walikuwepo.
Waliokuwepo ni pamoja na Ally Chocky, Kalala Jr, Chokoraa, Jojoo
Jumanne, James Kibosho, Miraji Shakashia, Victor Nkambi, Super Nyamwela,
Maria Soloma, Mapande na Chiku Kasika bila kusahau jeshi la kukodiwa J
Four Sukari.
Ally Chocky katika ndondo ya jana usiku
Khalid Chokoraa akiwajibika jukwaani
James Kibosho akicharaza drums na fulana yake ya Twanga Pepeta
Jojoo Jumanne kwenye bass
Kalala Jr akiwachezesha madansa wa Twanga
Kutoka kushoto ni Super Nyamwela, Chiku Kasika, Mapande na Maria Soloma
Miraji Shakashia na gitaa la solo
Victor Nkambi wa Twanga akipapasa kinanda jana usiku
Ally Chocky, Chokoraa, Kalala Jr na J Four Sukari
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/picha-8-za-wasanii-wa-twanga-pepeta.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/picha-8-za-wasanii-wa-twanga-pepeta.html
Copyright © saluti5