Header Ads

ad

Breaking News

Wizara yafunguka dawa mpya Yya Ukimwi




Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamis Kigwangallah

BAADA ya hivi karibuni dawa mpya ya kupambana na Virusi Vya UKimwi kugundulika na kuanza kutumika nchini Kenya, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini imefunguka, Uwazi lina habari kamili.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Msemaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Nsachris Mwamwaja alisema wao kama wizara wanafurahi kusikia dawa imepatikana lakini akafafanua kwamba bado haijaingia Tanzania.

Aliongeza kuwa kama dawa hiyo itapitia taratibu zote za usajili, wizara haina tatizo wala kipingamizi.
“Kwa sasa bado haijaingia Tanzania ila ikiingia tu tutawajuza wananchi ila lazima ipitie taratibu zetu za usajili baada ya hapo ndipo ianze kutumika,” alisema Mwamwaja.
www.mawingutz.blogspot.com
Baadhi ya wananchi nchini walionesha kufurahishwa na ujio wa dawa hiyo nchini Kenya wakiwa na imani kwamba zitaingia nchini na kusaidia waathirika wa Ukimwi.CHA 8 ZA WASANII WA TWANGA PEPETA WALIVYOJILIPUA JANA SIKU NA KUKAIDI AMRI YA BOSI WAO A+ A- Print Email Zaidi ya asilimia 80 ya wasanii wa Twanga Pepeta jana usiku walishiriki onyesho la pamoja na bendi ya taarab ya Wakali Wao ndani ya ukumbi wa Friends Corner Bar, Manzese jijini Dar es Salaam. Wasanii hao walishiriki onyesho hilo kinyume na amri ya bosi wao Asha Baraka ambaye hapo awali aliimbia Saluti5 kuwa haungi mkono wasanii hao kushiriki show hiyo. Asha Baraka akaenda mbali zaidi kwa kusema hata onyesho la Jumanne iliyopita baina ya bendi hiyo mbili, lilifanyika bila idhini yake. Kuelekea onyesho la jana, Asha Baraka akasema Twanga Pepeta haitashiriki onyesho hilo ambalo hapo awali lilitangazwa kuwa litakuwa likifanyika kila Jumanne ndani ya ukumbi huo wa Friends Corner huku likipewa jina la “Usiku wa Wababe”. Hata hivyo wasanii hao wa Twanga Pepeta walikuwa waungwana ambapo walitii amri ya bosi wao ya kutopeleka bendi (African Stars – Twanga Pepeta) na badala yake wakaenda kushiriki wao wenyewe bila jina la bendi wala vyombo vya bendi – karoso nyimbo tu. Naam nyimbo za Twanga Pepeta ndizo zilizosikika Friends Corner jana usiku ambapo mwimbaji na rapa Khalid Chokoraa akasikika akitupia rap inayosema: “hii ndondo, hii ndondo”. Mwimbaji Kalala Jr naye akachombeza: “Wazee wa Kujilipua, wazee wa kujitoa muhanga, kila Jumanne tuko hapa hata usiposikia tangazo, usiku kibabe Ndondo Jazz Band na Wakali Wao”. Kwa upande wake Ally Chocky yeye akasema: “Tukiwa kule ni Twanga Pepeta lakini tukiwa hapa sisi ni Wakali Wao Jazz Band kwahiyo kila Jumanne utakuwa unapata show ya Wakali Wao Modern Taradance na Wakali Wao Jazz Band”. Mmoja wa wasanii walioshiriki onyesho hilo akaiambia Saluti5 kuwa hawakukaidi amri ya bosi wao maana wao wamekwenda kama wasanii wa Twanga Pepeta na hawakwenda kama bendi ya African Stars “Twanga Pepeta”. “Tunamheshimu sana bosi wetu na kamwe hatuwezi kukiuka amri yake hasa ukizingatia kuwa Jumanne bendi yetu huwa haifanyi kazi,” alisema msanii huyo. Hadi kamera ya Saluti5 inaondoka ukumbini hapo, sura za wasanii wakubwa wa Twanga Pepeta ambazo hazikuonekana jukwaani ni Luizer Mbutu, Hajj BSS na God Kanuti, lakini mastaa wengine wote walikuwepo. Waliokuwepo ni pamoja na Ally Chocky, Kalala Jr, Chokoraa, Jojoo Jumanne, James Kibosho, Miraji Shakashia, Victor Nkambi, Super Nyamwela, Maria Soloma, Mapande na Chiku Kasika bila kusahau jeshi la kukodiwa J Four Sukari. Ally Chocky katika ndondo ya jana usiku Khalid Chokoraa akiwajibika jukwaani James Kibosho akicharaza drums na fulana yake ya Twanga Pepeta Jojoo Jumanne kwenye bass Kalala Jr akiwachezesha madansa wa Twanga Kutoka kushoto ni Super Nyamwela, Chiku Kasika, Mapande na Maria Soloma Miraji Shakashia na gitaa la solo Victor Nkambi wa Twanga akipapasa kinanda jana usiku Ally Chocky, Chokoraa, Kalala Jr na J Four Sukari

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2017/07/picha-8-za-wasanii-wa-twanga-pepeta.html
Copyright © saluti5

No comments