Thursday, July 20, 2017

PSG kuvunja rekodi kwa kumnunua Neymar pauni milioni 196

MARCO Verratti, Ousmane Dembele na Kylian Mbappe watakuwa kwenye mawindo ya Barcelona ikiwa timu hiyo itampoteza Neymar anayetajwa kutakiwa na Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa Daily Mail.


Taarifa zilizokuwepo awali zilitaja vigogo wawili wa England, Manchester United na Chelsea walikuwa wakihitaji huduma ya nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, lakini zilijitoa baada ya taarifa ya pauni milioni 196.

Klabu hizo zililalamika kwamba, PSG inajiamini kuwa na nafasi ya kuinasa saini ya Neymar na kumpeleka Ufaransa, wakati baba mnzazi wa nyota huyo akivuta subira mazungumzo na klabu yake.

Ingawa, ilishindwa kumsajili msimu uliopita kutokana na mambo yaliyojitokeza, imekuwa kimya kuhusu hatma yake.

Kwa mujibu wa GloboEsporte, Neymar aliwaambia wachezaji wenzake kutoka Brazil, Marquinhos, Lucas Moura, Thiago Silva na Dani Alves kwamba, ataungana nao Paris msimu ujao. 

No comments:

Post a Comment