Waziri Profesa Ndalichako afanya ziara mkoani Iringa

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela kushoto ni Mbunge wa jimbo la Iringa
mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako
amefanya ziara katika
shule za mkoani Iring zinazofundisha watoto wenye
mahitaji maalumu ikiwemo ya Makala wilayani Mfundi, Viziwi Mtwivila,
Sekondari ya Wasichana Mtwivila na Sekondari ya
Lugalo.
Leongo la ziara yake ni kukagua vifaa vya kufundishia vinavyotolewa na Serikali.
Joyce alipata fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu za shule hizo, ambapo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina
Masenza, Katibu Tawala wa mkoa huo, Wamoja Ayoub, Wakuu wa
wilaya ya Mufindi, Jamhuri David na Iringa Mjini, Richard
Kasesela.
Wengine walioambatana naye katika ziara hiyo ni mbunge wa Viti Maalumu mkoani humo, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mbunge wa Iringa Mjini,
Peter Msigwa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako kizungumza pamoja na viongozi
mbalimbali mkoani Iringa wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya
maalum ya viziwi mkoani humo

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa Iringa
mjini, Mchungaji Peter Msigwa katika Shule ya Viziwi, kulia ni
Mbunge Viti Maalumu, Zainab Mwamwindi na Mbunge wa Viti Maalumu Iringa, Ritha Kabati, wakiwaaangalia.
![]() |
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi nawalimu wakati wa ziara yake mkoani Iringa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako akiwa na wanafunzi wa Sekobdari ya Wasichana Iringa.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Joyve Ndalichako akizungumza na wananfunzi wa kidato cha tano wa Shule ya Sekondari Lugalo.
No comments